ABOODMSUNI NA SOKA LA BONGO: Villa watolewa na FFU; hawataki kuitwa vibonde

ABOODMSUNI NA SOKA LA BONGO: Villa watolewa na FFU; hawataki kuitwa vibonde: Baada ya mchezo wa Villa Squad FC vs Simba SC kumalizika na Villa kuwa vidume bin wababe. Mashabiki wa Simba SC, walitanda mlangoni wakis...
Read More

Villa squad 0 Azam fc 2


Villa 0 Azam 2

Villa Squad wameshindwa kubeba point tatu mbele ya Azam, baada ya kukubari  kufungwa magoli mawili kwa bila. katika mchezo uliomalizika jioni ya Leo Sep 13, 2011, huko Chamazi. 
Kwa matokeo hayo Azam anakuwa na point 8 huku Villa akibakiwa na 5 zake.
.
TimuPtsPWDLGFGAGD
Azam FC85221413
Villa Squad5511337-4

....habari hizi ni kwa msaada wa mtandao wa www.Kandanda.galacha.com/ asante
Read More

Villa squad vs Azam leo Chamazi

Katibu wa Villa Iddy Godigodi




Leo Septemba 13 Vijana machachari wa timu ya Soka ya Villa Squad wanatarajia kushuka dimbani kumenyana na wenyeji wao timu ya Azam FC, katika dimba hilo lililopo nje ya mji, Chamazi.  Mchezo huo utakua ni wa tano wa ligi kuu  ya Tanzania Bara..'VPL 2011-2012..


Bila shaka Vijana wa Villa Squad ambao walitoka kujeruhiwa goli moja katika mchezo wao ulipigwa mjini Tanga, uwanja wa Mkwakwani na kwa kufungwa bao 1, na Simba Sc, kwa mapumziko waliyopata na  mazoezi makali kutoka kwa kocha wao Abdala Msamba anayewanoa kwenye dimba la Villa lililopo viunga vya uwanja wa bonde la Jangwani.


Kikosi kamili cha Villa kimejiandaa vya kutosha kuakikisha wanaibuka na ushindi wa kishindo kwani wamedhamiria kufuta makosa yao katika mchezo huo hasa kutokana na kosa la mlinzi wao hata hivyo limefanyiwa kazi na watahakikisha wanaibuka na ushindi mnono.


"Leo ni lazima tufanye kile tulichofundishwa na kuakikisha Villa inafanya vizuri na kuzima ngebe za wapinzani wetu," alisema nahodha wa timu hiyo Shai Mpala.


Mpala pia alisema watahakikisha wanafanyia kazi mafundisho ya kocha na kuakikisha waleta ushindi dhidi ya Azam ambao mchezo wao wa juzi walitoka sare ya bila kufungana na Simba Sc.


Kwa upande wake Katibu mkuu wa timu hiyo Iddy GodiGodi alisema kikosi kipo imara na kinaendelea vizuri na hakuna majeruhi na pamoja uongozi umejiandaa kukabiriana kwa jambo lolote katika kuakikisha Villa inakua imara


(Imeandikwa na Afisa Habari wa Villa, Andrew Chale 0719076376,





Read More

Siku mabeki wa Villa Squad walivyomtoa nishai..Boban Mkwakwani...

...Kwa msaada wa mtandao wa Globalpublisher..
Read More

Simba Sc 1-0 Villa Squad Fc

Issa Mnally na Khatimu Naheka
BAO lililofungwa na mshambuliaji wa Simba, Gervais Kago, lilisababisha kuibuka kwa vurumai kubwa ndani ya Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga juzi Jumatano.

Vurumai hizo ziliibuka katika mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Villa Squad. Mashabiki wa Simba walianza kushangilia bao hilo lakini walikutana na upinzani mkali kutoka kwa wale waliokuwa wakiiunga mkono Villa.

Ghafla kulitokea mvutano na kukunjana mashati baina ya mashabiki wa Simba na wale wanaosemekana kuwa ni wa Yanga ambao hiyo juzi walikuwa wakiiunga mkono Villa.

Tafrani hizo ziliendelea kwa takribani dakika tano kabla ya mashabiki waungwana kujitokeza na kuwatuliza wenzao ambao hata baada ya kukubali waliendelea kutoleana lugha chafu, huku kila upande ukijigamba wao ni bora zaidi.

Katika mechi hiyo, Simba ilishinda kwa bao hilo moja lililofungwa katika dakika ya saba na raia huyo wa Afrika ya Kati.

Wakati huo huo, juzi kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro, mashabiki waliodaiwa kuwa ni wa Yanga waliugeuza uwanja huo kuwa sehemu ya mapambano baada ya kuwarushia mawe wenzao wa Simba waliokuwa wakiishangilia Mtibwa Sugar mara baada ya mechi hiyo.

Tukio hilo lilitokea baada ya mashabiki wa Yanga kuchukizwa na kutendo cha timu yao kutoka suluhu dhidi ya Mtibwa katika mechi hiyo ya ligi kuu.
Mashabiki hao walirusha mawe hayo wakati walipokuwa wakitoka uwanjani na kusababisha amani kupotea kwa dakika kadhaa.

Kutokana na tukio hilo, wachezaji na Kocha wa Mtibwa, Tom Olaba, waliokuwa wakijikusanya kabla ya kuondoka uwanjani hapo, walitawanyika na kuanza kukimbilia kwenye magari ili kujinusuru na mawe hayo.

Hata hivyo, hali hiyo ilitulia baada ya askari kuwatawanya mashabiki waliokuwa wakirusha mawe. Mpaka Championi Ijumaa linaondoka uwanjani hapo, hakukuwa na yeyote aliyejeruhiwa.

....kwa msaada wa mtandao wa globalpublishers.
Read More

VILLA SQUADS FC ‘Kambi moto’ NA MIKAKATI YA'VPL 2011-2012



      Yatamba  kufanya maajabu ligi kuu, watoa onyo kwa wanaowabeza.

Katibu Mkuu wa Villa Fc, Iddy Godigodi (kushoto) na Mjumbe wa kuteuliwa wa Villa fc, Ali Kindoile ( kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa kupokea vifaa kwa ajili ya ligi kuu ya msimu wa 2011-2012.


TIMU ya Villa Squad ‘Kambi moto’ imeapa kufanya vizuri kwenye msimu wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara na kuhakikisha inafanya majabu makubwa ambayo hayajafanywa na klabu yoyote katika historia ya soka nchini.
Katika mahojiano maalum na Villa,ama maalufu kama ‘Villa squad Kambi moto’ ambao  ni  timu pekee inayotokea Wilaya ya Kinondoni, ambao makazi yao pale Magomeni,Jijini Dar es Salaam, inajivunia usajili wa wachezaji bora na wazoefu.
Akielezea kwa undani juu ya malengo waliofikia ilikuakikisha wanasonga mbele, Katibu mkuu wa Villa, Idd Godigodi anaseema kuwa uongozi mzima kwa kushirikiana kwa pamoja wamejipanga kuakikisha wanafanya kila linalowezekana ili kushindana kwa hali ya juu.
Godigodi  anasema kuwa, miongoni ya mipango hiyo ni pamoja na kusajiri kikosi imara ambacho hakika kitaipeleka mbali timu hiyo ambayo kwa sasa kinanolewa na kocha msaidizi Said Chamosi, chini ya meneja wao Abdallah Msamba, akiwataja baadhi ya wachezaji wenye uzoefu kwenye klabu hiyo, nipamoja na
Nsa Job, Athuman Idd (Chuji), Aruna Shamte, Mohamed Kijuso, Idd Moshi na wengine wengi ambao wapo kwenye mazoezi kujiandaa na msimu wa ligi kuu.
Akielezea jinsi wanavyofarijika kiasi cha kujitamba kupambana kwenye msimu wa ligi kuu, Godigodi anasema kuwa, wachezaji,viongozi na mashabiki  wamebadirika  kwani kila mmoja anataka ushindi na wao wameamua kuleta mapinduzi.
“Villa ya mwaka huu ni ya tofauti kwani kila mmoja anaimani na timu na viongozi tumeamua kua kitu kimoja kufanikisha tunadumu misimu yote kama zilivyo  timu kongwe hapa nchini, hii ni timu kubwa aina tofauti  na Simba na Yanga, viongozi tumejipanga” anasema.
Akitoa pongezi kwa mashabiki kuwaunga mkono mpaka hapo alipofikia, alisema kuwa, wamelipa fadhira kwani watatumia uwanja  Chamazi unaomilikiwa na timu ya Azam fc, kama uwanja wao wa nyumbani.
“Kutokana na Villa kuwa na mashabiki wengi hasa Dar,  ni hakika watapata burudani ya kutosha hivyo waje kwa wingi pindi tutakapokuwa na michezo yetu pale Chamazi, Villa Kambi moto hakuna linaloshindikana” anasema.
 Alizitaka timu zinazoshiriki ligi kuu kuwa chonjo na wala wasiibeze kwani wao ni timu  imara na wala si ya wahuni kama wanavyoijua, hii ni kutokana na kuwa na uongozi makini hivyo kama wataendeleza imani hizo potofu wajue wataumia.
Akitoa, onyo juu ya baadhi ya viongozi wa soka nchini, ikiwemo shirikisho la mpira wa miguu, TFF, kwa vitendo vya kuwanyanyapaa na kuwaona kama wahuni huku wakiwahita wahuni, Godigodi anasema kuwa, wanataka heshima ishiko mkondo wake kwani klabu hiyo ni kongwe na inaongozwa na viongozi imara, hivyo ithaminiwe kama timu nyingine Duniani.

“Mwaka tupo ligi kuu Bara, na kila klabu iliyo ligi kuu ni mwanachjama wa TFF, sasa swala la kutuona sisi wahuni  linatoka wapi? Kama Villa ni wahuni mbona imetoa Makamu wa pili wa Rai wa shirikisho hilo, Nasibu” anasema Godigodi.

Aliendelea kusema kuwa,  viongozi hao waache kunyanyapa kwani wamekuwa wakifanya hivyo mara kwa mara na kuwaita wahuni wakati jambo si kweli na Villa inaeshimika ndani na nje ya  nchi na inawadhamini wake na wadau ambao walio na moyo wa kuendeleza soka la vijana hapa nchini.
Akielezea jinsi walivyopambana kwenye msimu wa ligi kuu 2008-2009, anasema kuwa kwenye msimu ule walikuwa wageni na hawakujiandaa vya kutosha ndio maana kwa bahati mbaya hawakufanikiwa kuendelea na ligi baada ya kushuka daraja lakini msimu huu huu wa 2011-2012 ndio mwisho wataendelea kubaki hadi dhamana kubwa ni kunyakua ubingwa ama kushika nafasi tatu za juu za ligi kuu.
“Siku zote unapotea wakati wa kwenda,lakini huwezi kosea njia ya kurudi, msimu huu Villa imerudi na itahakikisha haikosei kwani tuna timu ya kutosha na yenye  kufanya makubwa” anasema.

Timu ya Villa,  ilianzishwa mwaka 1973, huku ikiwa na wachezaji mbalimbali nyota ambao wengi walipata kuchezea timu kubwa za Simba na Yanga  sambamba na timu ya Taifa.
Msimu wa mwaka 2008/2009, Villa ilishuka daraja  hata hivyo baada hali hiyo iliweza kupambana  kwenye hatua ya ligi ya Taifa daraja la kwanza ambayo ilifanyika mkoani Tanga na kufanikiwa kupanda tena daraja la kwanza na kucheza ligi kuu 2011-2012, ambapo ilipanda pamoja na timu za  JKT Oljoro, Coastal Union  na  Moro United.

Mpaka sasa inawanachama wanaofikia  1000,  Pia inaundwa na viongozi wapya ambao ni pamoja na Kaimu mwenyekiti, Ramadhani Uledi, Mjumbe wa kamati ya Utendaji, Ally Kindoile,  Francis Komba (Mweka Hazina), Jumanne Said (Ofisa Habari ),kwa upande wa wajumbe  wa kuteuliwa  ni Ramadhani Soud na Yassin Masoud(awali alikuwa Katibu Mkuu kabla ya kujiuzulu kutokana na kutingwa na majukumu mengine).
Awali timu hiyo ilikuwa chini ya kocha mkuu, Juma Pondamali  ambaye alikuja kuiacha baadae.
Makala hii imeandaliwa na Andrew Chale,ambaye ni Afisa mpya wa habari wa Villa squad fc.. maoni, 0719076376,chalefamily@yahoo.com
Mwisho
Read More

VILLASQUAD KUJIACHIA CHAMANZI

Chuji aanza rasmi mazoezi Villasquad katika viwanja vya jangwani na ameonyesha uwezo mkubwa
Read More