About us

Villa Squad Foot ball Club ama maalufu kama "KAMBI MOTO" ni timu ya soka ya yenye makazi yake jijini Dar es Salaam-Magomeni-Mapipa. Ilianzishwa mwaka 1973 ikiwa kama taasisi maalum ya kuendeleza vipaji vya soka hivyo iliweza kuzalisha vijana kadhaa katika soka la Tanzania kutoka kipindi hicho mpaka sasa. Ilifanikiwa kuingia ligi kuu msimu wa 2008-2009, hata hivyo ilishuka daraja kufuatia maandalizi hafifu, lakini kutokana na kiu ya kutaka kuona inasonga mbele ilifanikiwa kupigana kwa hali na mali na mwaka huu wa 2010 iliweza kucheza michezo mbalimbali na kuifanikiwa kujiweka vizuri katika madaraja ya soka ya chini na hatimaye katika ligi ya Taifa ilifanikiwa kuingia ligi kuu kwa msimu huu wa 2011-2012. Hivyo ni hakika msimu huu wa 2011-2012 Villa imepania makubwa na kwa kufanikisha hilo limewataka wadau kujitokeza kuakikisha inafika mbali, hii ni pamoja na kujitokeza kusaidia udhamini wa hali na mali. "Villa FC, si timu ya wahuni ama watovu wa nidhamu kama wanavyodhani bali ni kama taasisi zingine za soka hapa nchini na Duniani kwa ujumla kwani tuna timu zaidi ya tatu, Under 14,17 21 na hii ya iliyopo ligi kuu...Villa squad fc daima mpira kwa Tanzania...
Read More