Thursday, September 8, 2011

VILLA SQUADS FC ‘Kambi moto’ NA MIKAKATI YA'VPL 2011-2012



      Yatamba  kufanya maajabu ligi kuu, watoa onyo kwa wanaowabeza.

Katibu Mkuu wa Villa Fc, Iddy Godigodi (kushoto) na Mjumbe wa kuteuliwa wa Villa fc, Ali Kindoile ( kulia) wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa kupokea vifaa kwa ajili ya ligi kuu ya msimu wa 2011-2012.


TIMU ya Villa Squad ‘Kambi moto’ imeapa kufanya vizuri kwenye msimu wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara na kuhakikisha inafanya majabu makubwa ambayo hayajafanywa na klabu yoyote katika historia ya soka nchini.
Katika mahojiano maalum na Villa,ama maalufu kama ‘Villa squad Kambi moto’ ambao  ni  timu pekee inayotokea Wilaya ya Kinondoni, ambao makazi yao pale Magomeni,Jijini Dar es Salaam, inajivunia usajili wa wachezaji bora na wazoefu.
Akielezea kwa undani juu ya malengo waliofikia ilikuakikisha wanasonga mbele, Katibu mkuu wa Villa, Idd Godigodi anaseema kuwa uongozi mzima kwa kushirikiana kwa pamoja wamejipanga kuakikisha wanafanya kila linalowezekana ili kushindana kwa hali ya juu.
Godigodi  anasema kuwa, miongoni ya mipango hiyo ni pamoja na kusajiri kikosi imara ambacho hakika kitaipeleka mbali timu hiyo ambayo kwa sasa kinanolewa na kocha msaidizi Said Chamosi, chini ya meneja wao Abdallah Msamba, akiwataja baadhi ya wachezaji wenye uzoefu kwenye klabu hiyo, nipamoja na
Nsa Job, Athuman Idd (Chuji), Aruna Shamte, Mohamed Kijuso, Idd Moshi na wengine wengi ambao wapo kwenye mazoezi kujiandaa na msimu wa ligi kuu.
Akielezea jinsi wanavyofarijika kiasi cha kujitamba kupambana kwenye msimu wa ligi kuu, Godigodi anasema kuwa, wachezaji,viongozi na mashabiki  wamebadirika  kwani kila mmoja anataka ushindi na wao wameamua kuleta mapinduzi.
“Villa ya mwaka huu ni ya tofauti kwani kila mmoja anaimani na timu na viongozi tumeamua kua kitu kimoja kufanikisha tunadumu misimu yote kama zilivyo  timu kongwe hapa nchini, hii ni timu kubwa aina tofauti  na Simba na Yanga, viongozi tumejipanga” anasema.
Akitoa pongezi kwa mashabiki kuwaunga mkono mpaka hapo alipofikia, alisema kuwa, wamelipa fadhira kwani watatumia uwanja  Chamazi unaomilikiwa na timu ya Azam fc, kama uwanja wao wa nyumbani.
“Kutokana na Villa kuwa na mashabiki wengi hasa Dar,  ni hakika watapata burudani ya kutosha hivyo waje kwa wingi pindi tutakapokuwa na michezo yetu pale Chamazi, Villa Kambi moto hakuna linaloshindikana” anasema.
 Alizitaka timu zinazoshiriki ligi kuu kuwa chonjo na wala wasiibeze kwani wao ni timu  imara na wala si ya wahuni kama wanavyoijua, hii ni kutokana na kuwa na uongozi makini hivyo kama wataendeleza imani hizo potofu wajue wataumia.
Akitoa, onyo juu ya baadhi ya viongozi wa soka nchini, ikiwemo shirikisho la mpira wa miguu, TFF, kwa vitendo vya kuwanyanyapaa na kuwaona kama wahuni huku wakiwahita wahuni, Godigodi anasema kuwa, wanataka heshima ishiko mkondo wake kwani klabu hiyo ni kongwe na inaongozwa na viongozi imara, hivyo ithaminiwe kama timu nyingine Duniani.

“Mwaka tupo ligi kuu Bara, na kila klabu iliyo ligi kuu ni mwanachjama wa TFF, sasa swala la kutuona sisi wahuni  linatoka wapi? Kama Villa ni wahuni mbona imetoa Makamu wa pili wa Rai wa shirikisho hilo, Nasibu” anasema Godigodi.

Aliendelea kusema kuwa,  viongozi hao waache kunyanyapa kwani wamekuwa wakifanya hivyo mara kwa mara na kuwaita wahuni wakati jambo si kweli na Villa inaeshimika ndani na nje ya  nchi na inawadhamini wake na wadau ambao walio na moyo wa kuendeleza soka la vijana hapa nchini.
Akielezea jinsi walivyopambana kwenye msimu wa ligi kuu 2008-2009, anasema kuwa kwenye msimu ule walikuwa wageni na hawakujiandaa vya kutosha ndio maana kwa bahati mbaya hawakufanikiwa kuendelea na ligi baada ya kushuka daraja lakini msimu huu huu wa 2011-2012 ndio mwisho wataendelea kubaki hadi dhamana kubwa ni kunyakua ubingwa ama kushika nafasi tatu za juu za ligi kuu.
“Siku zote unapotea wakati wa kwenda,lakini huwezi kosea njia ya kurudi, msimu huu Villa imerudi na itahakikisha haikosei kwani tuna timu ya kutosha na yenye  kufanya makubwa” anasema.

Timu ya Villa,  ilianzishwa mwaka 1973, huku ikiwa na wachezaji mbalimbali nyota ambao wengi walipata kuchezea timu kubwa za Simba na Yanga  sambamba na timu ya Taifa.
Msimu wa mwaka 2008/2009, Villa ilishuka daraja  hata hivyo baada hali hiyo iliweza kupambana  kwenye hatua ya ligi ya Taifa daraja la kwanza ambayo ilifanyika mkoani Tanga na kufanikiwa kupanda tena daraja la kwanza na kucheza ligi kuu 2011-2012, ambapo ilipanda pamoja na timu za  JKT Oljoro, Coastal Union  na  Moro United.

Mpaka sasa inawanachama wanaofikia  1000,  Pia inaundwa na viongozi wapya ambao ni pamoja na Kaimu mwenyekiti, Ramadhani Uledi, Mjumbe wa kamati ya Utendaji, Ally Kindoile,  Francis Komba (Mweka Hazina), Jumanne Said (Ofisa Habari ),kwa upande wa wajumbe  wa kuteuliwa  ni Ramadhani Soud na Yassin Masoud(awali alikuwa Katibu Mkuu kabla ya kujiuzulu kutokana na kutingwa na majukumu mengine).
Awali timu hiyo ilikuwa chini ya kocha mkuu, Juma Pondamali  ambaye alikuja kuiacha baadae.
Makala hii imeandaliwa na Andrew Chale,ambaye ni Afisa mpya wa habari wa Villa squad fc.. maoni, 0719076376,chalefamily@yahoo.com
Mwisho

0 comments:

Post a Comment